Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula amebainisha hayo katika mkutano wa hadhara kata ya Igogo hivi leo katika mwendelezo wa Ziara zake kata 18 za halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kukagua Miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi sanjari na kutoa mrejesho wa wa taarifa ya Bunge la bajeti.

Mhe Mabula amesema serikali imekamilisha ujenzi ma barabara kwa kiwango cha rami yenye urefu wa Kilometa 0.2  itokayo TANESCO kwanzia barabara kuu la Kenyatta kuelekea  Mrungushi yenye thamani ya shilingi 71,000,000.00. Katika sekta ya elimu serikali imewezesha  ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za Msingi. Kadharika Mhe Mabula ameelezea nia ya serikali kuboresha mazingira ya makazi hatarishi ambapo Kata ya Igogo ina Kaya 1287 kati ya Kaya 3360 zilizonufaika na mpango wa Ujenzi wa Vyoo bora, pamoja na Mtandao wa maji taka uliogharimu shilingi 1,041,073,366. 

Mhe Mabula akijibu maswali ya Papo kwa Papo amefafanua kwamba, serikali imedhamilia kuboresha sekta ya Afya ambapo Fedha ya dawa na vifaa tiba imeongezeka toka 47%-98% Nyamagana. Natayari imeweka mkakati wa ujenzi wa wodi ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya Kata, lakini tayari Zahanati hiyo imeboreshwa kwa uwezekaji wa dari jipya pamoja na usanifu wa sakafu kwa vigae. Mhe Mabula amemalizia kwa kugusia utatuzi wa kero ya Ardhi ambapo serikali  inaweka mkakati wa wananchi kunufaika na Mpango Kabambe utawaweza urasimishaji wa maeneo yao kwa upimaji shirikishi.

Mkutano huu uliudhuliwa katibu wa Chama Cha Mapinduzi Nyamagana, Mwenezi wilaya, Diwani mwenyeji Jonathan Minja, na Diwani Kata ya Mkuyuni Mhe Donator Gappi, Diwani Viti Maalum Mhe Mama Jeremiah, Viongozi wa CCM kata na matawi pamoja na watendaji wa Kata na Mitaa.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: