Na Lorietha Laurence-WHUSM,Mbulu Mjini
Serikali  imeandaa mpango wa kuwaenzi watu  mashughuri  wakiemo wanamichezo wakongwe  ambao wamewahi kuliletea taifa heshima katika mashindano mbalimbali  akiwemo mwanariadha Mkongwe Bw. John Steven Akwhari.

Hayo yamesemwa leo Mbulu Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza alipomtembelea mwanariadha huyo nyumbani kwake  ambapo alipata fursa ya kuona medani , tuzo na vikombe alivyowahi kushinda mwanariadha huyo.

“ Sisi kama Wizara tumeanzisha kampeni ya Uzalendo ambapo mwaka jana  tuliwaenzi wasanii wa zamani wa muziki na mwaka huu  mnamo Oktoba 14 ni zamu ya wanamichezo wakongwe akiwemo Bw. John Akwhari ” amesema Mhe. Shonza

Alizidi kueleza kuwa amevutiwa na jinsi mwanariadha huyo anavyotunza kumbukumbu zake huku akiwataka wanamichezo na watu  wengine kuiga mfano huo bora ili kuviwezesha vizazi vijavyo kupata historia nzuri katika sekta ya michezo.

Naye Mwanariadha Mkongwe Bw. John Steven Akwhari amesema amefurahi kuona Serikali inatambua na kuthamini mchango wake katika sekta ya michezo na kuhaadi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kwa pamoja kuleta maendeleo katika sekkta hiyo muhimu.

 Bw. John Akwhari ni mwanariadha wa zamani wa Tanzania  wa kwanza  kufungua milango ya kushiriki riadha nje ya nchi ambapo alijizolea umaarufu katika mashindano ya mwaka 1968  ya Olimpiki nchini Mexico ambapo licha ya kuwa wa mwisho aliueleza umati kuwa nchi yake ilimtuma kumaliza mbio na siyo kuanza mbio.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: