Baba mdogo wa marehemu, Patrick Peter, Bazo Komu amefafanua sababu ya mama mzazi wa mtoto huyo Rose Alphonce 'Muna Love' kuondoka uwanja wa ndege akiwa na dokumenti zitakazosaidia mwili wa mtoto wake kuchukuliwa katika uwanja wa ndege ni kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo.

Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere, Bw. Bazo amesema hilo limetokea baada ya mwanamama huyo kupoteza nguvu baada ya kushuka uwanjani hapo na wao kumuingiza kwenye gari pasipo kukumbuka kuchukua dokumenti hizo.

Bazo ameweka wazi kwamba hakuna tatizo lingine ambalo lingesababaisha wao kushindwa kuuchukua mwili wa mtoto kwa kuwa mambo yote yalishapangwa na hakuna tafrani yoyote inayoendelea kuhusiana na mtoto wapi akazikwe.

"Hakuna tatizo lolote, wala hapakuwa na makubaliano ya mtoto azikwe wapi kwa sababu tunajua mama ni nani na baba ni yupi. Kitu kilichotokea ni kwa sababu wote tumemuona Muna hali yake ilivyo. Ameshuka hajiwezi, imebidi ashikiliwe ili aweze kutembea. Tumejisahahu kuzichukua hizo dokumenti baada ya kumuingiza kwenye gari. Na kwa hali ya kawaida huwezi kuingia kwenye pochi ya mwanamke kukagua" amefafanu Bazo.

Ameongeza, "Kwa sasa tunafanya utaratibu wa kujua jinsi gani hizo dokumenti zitafika hapa ili tuweze kuuchukua mwili wa mtoto tuweze kuendelea na taratibu zingine"
Share To:

msumbanews

Post A Comment: