Na Rhoda Ezekiel Kigoma

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ameyataka mashirika pamoja na vikundi vya wakimbizi vinavyo washawishi wakimbizi kuacha kujiandisha kurudi kwao kwa hiyari kuacha tabia hiyo.

Mkuu huyo aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wakimbizi katika kambi ya Ndita wilayani Kibondo ambapo amesema mashirika na vikundi hivyo wanavijua endapo wataendelea na tabia hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

"Mashirika yanayo chochea wakimbizi na kuunga mkono upinzani nchini Burundi yataondolewa na hayata ruhusiwa kutoa huduma tena," amesema.Ameongeza kwa sasa hali ya amani na usalama kwa nchi ya Burundi ni salama na mali walizoziacha kwao bado zipo,hivyo wakimbizi warejee nyumbani kwao kwani hakuna utaratibu wa mkimbizi wa Burundi kwenda nchi ya tatu utaratibu huo ni kwa Wakongomani pekee.

AmesemakKambi ya wakimbizi sio mahali pa kudumu ni mahali pa kuhifadhi raia ambao nchini mwao kuna utishio wa kiusalama.Kwa sasa Burundi usalama upo hivyo wananchi wana wanatakiwa kurejea nchini kwao kwa hiyari na kusitokee vitisho wala ushawishi wowote.

"Utaratibu wa kuwapeleka raia wa Burundi nchi ya tatu ni ya haupo na Serikali ya Tanzania haitoi uraia kwa wakimbizi wa Burundi kama njia zote zimefungwa njia iliyopo ni moja tu mrejee kwenu kwa hiyari na UNHCR na IOM itahakikisha mnasafiri na mnafika kwenu mnaishi vizuri," amesema Brigedia Jenerali Maganga.

"Yapo mashirika shirika yana kwamisha mchakato huu tunawajua, niwaombe kitu kimoja kama mna maslahi yenu binafsi muyaweke pembeni hatuta wavumilia, ukiona shirika lako limeitwa ofisini kwangu jiandae kuondoka na tukifukuza hapo hakuna sehemu tena kstika Tanania hii utafanya kazi," alielezea Maganga.

Pamoja na hayo baadhi ya wakimbizi akiwemo Nkruliyabanzi Andrew amesema wao kama wakimbizi wanapenda kurejea nchini mwao lakini bado wanauoga kuwa wanaweza kurudi nchini mwao wakaanza kunynyaswa kwakuwa walikimbia.Waliomba Serikali ya Tanzania kuzungumza na Serikali ya Burundi kuingia kambini kuzungumza na wakimbizi na kuwahahikishia endapo watarudi wataishi salama wao wako tayari kurejea nchini mwao wakihakikushiwa hayo.

Uamuzi wa kuwarejesha wakimbizi walioingia nchini Tanzania 2015 ulifikiwa Mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo pande tatu za shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR na nchi za Burundi na Tanzania kujiridhisha hali ya usalama Burundi imerejea na kuwaomba Wakimbizi warudi kwao ambapo mpaka sasa baadhi ya wakimbizi wamerejea nchini mwao kwa hiyari.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga akizungumza na wakimbizi katika kambi ya Nduta wilayani Kibondo Mkoani Kigoma akiwataka kurejea Nchini kwao kwa hiyari, pembeni ni watumishi wa idara ya mambo ya ndani na Baadhi ya mashirika ya kuhudumia wakimbizI.
Baadhi ya Wananchi  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga alipokuwa akizungumza na wakimbizi katika kambi ya Nduta wilayani Kibondo Mkoani Kigoma akiwataka kurejea Nchini kwao kwa hiyari.
 Burudani ya ngoma ilikuwepo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: