Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekanusha taarifa za chama hicho kumpa barua ya onyo mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

Akizungumza leo Alhamisi Julai 5, 2018 Polepole amesema mbunge huyo wa CCM hajapewa barua ya onyo, kwamba chama hicho tawala kina taratibu zake.

Taarifa za Nape kupewa barua hiyo zimesambaa mitandaoni huku mwenyewe akikanusha kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Taarifa hizo zilitiwa chumvi zaidi baada ya kuhusishwa na msimamo wa Nape katika suala la Korosho lililoibuka katika Bunge la Bajeti.

Katika mkutano huo wa Bunge, Nape na wabunge wenzake kutoka mikoa ya Kusini walipinga uamuzi wa Serikali wa kubadilisha Sheria ya Korosho, ikiwa ni pamoja na fedha za ushuru wa korosho kwenda katika mfuko mkuu wa Hazina.

Akizungumza baada ya uwasilishwaji wa ripoti ya taasisi ya Twaweza jijini Dar es Salaam, Polepole amesema chama hicho tawala kina utaratibu wa vikao linapotokea tatizo la mwanachama wake
Share To:

msumbanews

Post A Comment: