Thursday, 12 July 2018

Peter Amtuhumu Muna Kwa Kusambaza Picha Zake Chafu Mtandaoni

Mzazi mwenza wa Muna anayejulikana kama Peter Zachariah amemjia juu mzazi mwenzake na kudai yeye ndiye mtu  aliyehusika kwa usambazaji wa picha zake Chafu Kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Peter alidai kuwa anajua wazi anayezisambaza picha hizo mitandaoni ni Muna kwa nia ya kumchafua kwa sababu Aprili, mwaka huu alirudi nyumbani kwake Mwananyamala-Kisiwani na kujifanya kuwa anapanga vitu vyake ndani ya nyumba hiyo kumbe nia ni kunasa picha hizo.
 
"Unajua chochote kinachoendelea hivi sasa najua wazi ni mpango wa Muna, anajitahidi kuufanya ili mimi nionekane wa ajabu baada ya kuona watu walivyonichukulia tofauti kwenye kipindi chote cha msiba wa mtoto wetu hivyo anataka kunichafua lakini mimi kwa hilo sitetereki“.

Peter amekiri alikuwa Kwenye Mahusiano na mwanamke huyo baada ya kuachana na Muna na kumtaja kwa jina la Rehema na kudai kuwa Muna anamfahamu mwanamke huyo.

"Kinachonishangaza mimi Muna anataka kujifanya huyo mwanamke ni mpya kwake lakini sio kabisa, anajua kila kitu na jinsi alivyokuwa akitangatanga kwa wanaume tofautitofauti, mimi ningeishi vipi kama mwanaume? Nafikiri anajua fika kwa kufanya hivyo atanichafua mimi kumbe anajichafua yeye”.

Mgogoro wa Muna na mumewe ulijulikana hadharani hivi karibuni mara baada ya mtoto wao kipenzi Patrick kufariki nchini Kenya alipokuwa amekwenda kutibiwa.

Mara baada ya Patrick kufariki, mjadala mzito uliibuka mitandaoni ambapo kuna baadhi walisema baba yake ni Mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson aliyewahi kuwa mpenzi wa Muna lakini wengine wakasema ni wa Peter.

Muna alipotafutwa atoe neno kuhusu tuhuma hizo hakupatikana haraka. Siku chache zilizopita Muna alitangaza atafanya mkutano na waandishi wa habari na kujibu tuhuma zote.

No comments:

Post a comment