Wednesday, 4 July 2018

Mwili wa Prof. Maji Marefu wawasili Karimjee kwa ajili ya kuagwa


MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Stephen Ngonyani “Profesa Majimarefu” umewasili katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam asubuhi hii kwa ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kupelekwa Korogwe mkoani Tanga kwa mazishi.

Mwili wa Ngonyani umewasili kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti, Hiospitali ya Taifa Muhimbili leo Jumatano, JUlai 4, 2018 majira ya saa nne na shughuli ya kuaga ikaanza ikiwemo salam za rambirambi na ibada ya kuaga.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na vya kijamii na viongozi wa dini wameungana na wabunge wenzake na marehemu pamoja na wananchi kutoa heshima zao za mwili kwa mwili wa marehemu.

Profesa Majimarefu aliaga dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya taifa Muhimbili jijini dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment