MKAZI wa mtaa wa Starehe wilayani Tarime mkoani Mara ambaye ni mwenyekiti wa Jumuia ya umoja wa vijana Chama cha mapinduzi UVCCM wilayani hapa, Godfrey Fransic 30 amefikishwa mahakama ya wilaya kwa kosa la mitandao.

Akisomewa shitaka linalo mkabili mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Tarime Veronica.

Mugendi Mwendesha Mashitaka wa jeshi la Polsi Kazeni Mrita aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 1,Julai ,2018 majira ya mchana mtuhumiwa  mwenye kesi Na. 315 alisambaza taarifa zisizo rasmi kwa kutuma ujumbe  kwa njia ya mtandao kinyume cha sheria ya mtandao.

Mrita aliiambia mahakama hiyo kuwa taarifa hiyo ilisema kuwa ‘’Tunamshukuru Mungu muumba mbingu na nchi Peter Zakari mmiliki wa mabasi ya Zakaria yanayofanya safari za Tarime Mwanza amewazidi nguvu watekaji baada ya kufanikiwa kuwajeruhi watekaji wawili kwa risasi.

Mji wa Tarime Umerindima na vijana wamejipanga kila kona ya mji huo kuhakikisha kuwa watekaji hao hawachomoki, kwa sasa tuko Polisi wasiojulikana hatimaye wamejulikana, Mungu ndiye anayepanga nani afe na kwa wakati gani na si wewe unaeamua, By Godfrey Francins Mwenyekiti wa Vijana wa CCM wilaya ya Tarime na hivyo kusababisha Kupotosha”alisema..

Hakimu Mugendi alimuuliza mtuhumiwa kama ni kweli ambapo Mtuhumiwa alijibu mbele ya mahakama hiyo kuwa  si kweli.

Wakili wa mtuhumiwa huyo Onyango Otyeno wakampuni ya  Zamazon aliiomba mahakama hiyo kumpa mteja wake dhamana kwasbabu kosa leneywe lina dhamana.

Hakimu Mugendi  alitoa masharti ya dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja kwa masharti ya  sh.milioni 2 kwa maneno kila mmoja na vitambulisho na barua za vitambulisho nakwamba mshitakiwa amedhaminiwa hivyo ni wajibu wadhamini kuhakikisha  msitakiwa anafika mahakamani anapohitajika..

Hata hivyo wadhamini walikidhi vigezo ambao ni Joel Mwita mkazi wa kijiji cha Sokoni kata ya Sirari na Yusuph Biarusi mkazi wa Mtaa wa Starehe Kata ya Nyamisangura.

Mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana na kesi yake inayomkabili namba 315/018 itatajwa tena mahakamani hapo  30,Julai 018.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: