Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndg.Saitoti Zelothe Akivalishwa Skafu kwa kukaribishwa Meru.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru Timotheo Mnzava Akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndg. Saitoti Zelothe pomoja na Kamati ya Utekelezaji Vijana Mkoa.
Mjumbe wa Baraza kuu  Taifa Bi. lulu Mwacha Akiteta jambo na Mwenyekiti wa Uvccm Ndg. Saitoti Zelothe.
Moja ya shamba linalomilikiwa na Umoja wa Vijana wa Ccm Meru.

Mwenyekiti waUmoja wa Vijana Ccm (Uvccm) Mkoa wa Arusha Ndugu Saitoti Zelothe, Sambamba na Kamati ya Utekelezaji Mkoa wameendelea na ziara yao Meru ambapo wamekagua shughuli mbalimbali za Kimaendeleo ikiwemo zoezi la uwezeshaji wa vijana katika wilaya hiyo ikiwa ni Pamoja na mashamba,viwanja na nyumba za biashara vinavyomilikiwa na Jumuiya hiyo.

Ndugu Saitoti amekutana na Vijana wa CCm,Viongozi wa Chama na Serikali na Ametembelea miradi mbalimbali ya Vijana na amepokea Taarifa kazi ya Ofisi ya Vijana Wilaya.

Pia Mwenyekiti amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli na kuwataka vijana kuenzi kazi hiyo kwa kuwa wazalendo na wachapakazi zaidi katika nyanja mbalimbali walizopo.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Bi Lulu mwacha amewataka Vijana kuendelea kujitolea katika kazi za kijamii ili kuendelea kusambaza ujumbe Mkubwa kwa wananchi kwa kukitetea chama cha Mapinduzi Ccm huku akiwsihi Vijana hao wa Meru kuunda kikundi cha Ujasiriamali na kuanza kutumia mradi wa shamba linalomilikiwa na umoja wa Vijana lenye hekari  kumi na moja ili kuanza kulima kilimo cha kisasa.

Mwenyekiti wa Uvccm Ndugu Saitoti Zelothe Atakamilisha ziara yake katika Wilaya ya Ngorongoro.

Omary Lumato
Katibu 
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi


Share To:

msumbanews

Post A Comment: