Monday, 16 July 2018

Mwanajeshi wa JWTZ Akutwa Amefariki Kisimani

Polisi Mkoa wa Kusini Unguja imesema inaendelea na uchunguzi kubaini sababu za kifo cha askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambaye mwili wake ulikutwa kisimani.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Suleiman Hassan Suleiman alisema jana kuwa wanaendelea na uchunguzi, huku akimtaja mwanajeshi huyo kuwa niOthman Khatib Othman (36), mzaliwa wa kisiwani Pemba.

Suleiman alisema Alhamisi jioni wiki iliyopita, walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa kuna mwili umeonekana kisimani.

Alisema kisima hicho kipo eneo la Ubago jirani na kambi ya JWTZ alikokuwa akifanya kazi na kwamba, mwili uliopolewa Ijumaa saa 11:45 asubuhi.

Kamanda Suleiman alisema baada ya uchunguzi mwili ulizikwa eneo jirani kutokana na kuharibika, hivyo kushindikana kusafirishwa kupelekwa nyumbani kwao.

No comments:

Post a Comment