Wednesday, 4 July 2018

Msajili aliyesimamishwa Kazi na Nchemba arudishwa Kazini


MSAJILI wa Taasisi za Kiraia na Vyama vya Hiari wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Merlin Komba, ambaye alisimamishwa kazi na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba,  wiki chache zilizopita kufuatia msajili huyo kuandika barua kwa kanisa la KKKT kutaka lifute waraka wake wa Pasaka, amerudishwa kazini.

Siku moja tu baada ya Lugola kuapishwa, Komba amerudishwa kazini. Hata hivyo Lugola amekataa kusema ni nani aliyemrudisha kazini msajili huyo, na kwa utaratibu gani.

Mwigulu alisema barua hiyo kwenda KKKT iliandikwa na ‘wahuni’ waliokuwa na lengo la kuhatarisha amani ya nchi.

No comments:

Post a Comment