Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza siku ambayo uchaguzi mdogo wa marudio wa ubunge na udiwani katika kata 79 na jimbo moja utafanyika.
Uchaguzi huo unafanyika Tanzania Barakufuatia Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kuwa wazi baada ya aliyekua Mbunge wake, Kasuku Bilago kufariki pamoja na Kata 79 kutokuwa na madiwani kulikotokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujiuzulu kwa madiwani hao.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchuguzi (NEC), Athuman Kihamia amesema uchaguzi huo utafanyika August 12, 2018 ambapo fomu za uteuzi zimeana kutolewa July 8 hadi ifikapo July 14, 2018 huku Kampeni za uchaguzi huo zitaanza July 15, 2018 hadi August 11, 2018.
“Uchaguzi huu mdogo wa Ubunge utahusisha Jimbo la Buyungu na udiwani kwenye Kata 79 zilizopo Halmashauri 43 kwenye mikoa 24 ya Tanzania Bara” amesema Kihamia
” Kutakuwa na wasimamizi wa uchaguzi 44, wasimamizi wasaidizi ngazi ya Jimbo 88 na maafisa uchaguzi 44, wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata wanatarajiwa kuwa 184 na kwa upande wa vituo vya kupigia kura kutakuwa na vituo 1601″ Kihamia
Share To:

msumbanews

Post A Comment: