Thursday, 26 July 2018

MKURUGENZI MBULU AGAWA BAISKELI KWA WALEMAVU

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga ametoa msaada wa baiskeli sita kwa ajili ya walemavu ili kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku. Kamoga amewashukuru marafiki zake waliochangia katika kuboresha maisha na kuwasaidia wananchi wanyonge.

Kamoga amesema “Serikali hii inawajali wanyonge na sisi kama viongozi lazima pia tufikiri zaidi ya ukomo wa kazi zetu za kila siku katika kuwahudumia wananchi wa hali ya chini. Nafasi hii niliyopewa na Mungu kupitia kwa Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli ni kwa ajili ya kuwatumikia na kuwasaidia watanzania hasa wanyonge,nafasi hii ni kwa ajili ya watu ninaotakiwa kuwatumikia na si kwa ajili yangu binafsi,ndio maana ya utumishi”alisema Kamoga.

Baiskeli hizo zimetolewa na marafiki wa mkurugenzi huyo wanaotambua mchango wake katika kulitumikia taifa na kuwajali watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, Wadau hao wameahidi kutoa vifaa vingine kila watakapokuwa na uwezo wa kifedha ili kusaidia jamii inayoishi kwenye mazingira magumu Wilayani Mbulu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akipozi kwa picha na Mzee Malkiadi Bura kutoka kata ya Masqaroda ambaye ni mlemavu wa miguu baada ya kumkabidhi baiskeli maalum kwa ajili ya kutumia katika shughuli zake wananchi walemavun wengine waliokabidhi wa baiskeli hizo ni kutoka kata za Tumati, Maghang, na Dinamu Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akipiga picha ya pamoja na dada Rose Boay kutoka Haydom baada ya kumkabidhi baiskeli yake leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akipiga picha ya pamoja na mama Maria Chacha kutoka kata ya Haydom baada ya kumkabidhi baiskeli yake leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akiwa na wananchi wa Mbulu wenye ulemavu wa miguu aliowakabidhi baiskeli maalum kwa ajili ya matumizi katika shughuli zao za kila siku
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akijadiliana jambo na baadhi ya viongozi huku mama Maria Chacha kutoka kata ya Haydom kushoto na dada Rose Boay kutoka Haydom wakiwasikiliza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na walemavu aliowapatia baiskeli.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: