Tuesday, 3 July 2018

Meya wa Dar akubaliana na Meya wa Liuzhou kushirikianaMstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita anatarajia kuwakutanisha wahandisi wa Tanzania na wale wa China katika kupanga maeneo ya kutengeneza barabara na reli.

Hayo yamejiri leo baada ya Meya Mwita kukutana na kufanya mazungumzo na Naibu Meya wa Jiji la  Liuzhou, Dk. Liu Ke ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kushirikina katika sekta ya biashara.

Meya Mwita amefafanua kuwa ugeni huo wa Naibu Meya uliokuwa na watu saba, wamekubaliana pia kusaidia katika suala la ujenzi wa barabara na kwamba jiji la Dar es Salaam limewakaribisha.

Meya amesema mbali na ushirikiano huo, ugeni huo umemualika Meya   Mwita kwenda kujifunza namna ambavyo wamefanikiwa katika Teknolojia ya kuendesha magari kwa kutumia nishati ya umeme.

“Leo tumepata ugeni kutoka jiji la Liuzhou ,tumezungumza mambo mengi, na mfahamu kuwa wamekuwa ni marafiki zetu kwa muda mrefu, hasa kwenye ujenzi wa miundombinu mbalimbali, na hivi sasa wameahidi kutusaidia kujenga barabara jijini hapa. Lakini pia wametupongeza kutokana na namna ambavyo jiji letu limejengeka ,yapo mambo mengi ya kuvutia jijini hapa, lakini wametualika kwenda kuona magari yanayotumia umeme, na sisi tutakwenda” amesema Meya Mwita.

Kwa upande wake, Dk. Kiu Le amempongeza Meya Mwita nakusema kuwa watazidi kuimarisha urafiki uliopo sambamba na kusaidia ujenzi wa reli, barabara, nakutoa misaada mingine mbalimbali.

Amesema kuwa jiji la Liuzhou linauwezo wa kukidhi mahitaji ya wananchi wa jijini hapa na kwamba wako tayari kutoa ushirikiano wao kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment