Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula hivi Leo ameenza ziara ya kikazi katika Kata kumi na nane za halmashauri ya Jiji la Mwanza akianzia Kata ya Isamilo katika Kata kumi na mbili za mwanzo kuelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi 2015-2020. Ziara italenga kutembelea miradi ya Maendeleo, kusikiliza kero za Wananchi katika mikutano ya hadhara sanjari na kutoa mrejesho kwa wananchi wa Bunge la bajeti.

Mhe Mabula amewaambia wananchi katika ahadi alizo waahidi wananchi wa kata hiyo ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara na tayari ameisimamia serikali katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha rami kata hiyo yenye urefu wa kilometer 0.6 sanjari  na barabara ingine ya mawe yenye urefu wa kilometers 2.9 itakayogharimu shilingi billion 1.1 na katika mwaka huu wa fedha serikali imetoa shilingi 700,000,000 kwaajiki ya kuanzia na ujenzi huo kwa kilometers  1.8.

Mhe Mabula amefafanua kuwa hadi sasa serikali imeboresha sekta ya elimu katika shule zote mbili za Msingi katani humo na Mfuko wa Jimbo umewezesha ukarabati wa madarasa ili kutekeleza Ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi unaoelekeza elimu Bule kwa vitendo. Kadharika katika kukabiliana na changamoto ya maji kwa kauli Mbiu ya kumtua ndoo mwanamke tayari ujenzi wa tank kubwa la maji umeanza lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita 1,200,000.

Akijibu maswali ya papo kwa papo kuhusu sekta ya Afya kutoka kwa wananchi Mhe Mabula amewaambia wananchi serikali imetoa shilling 122,000,000 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati ya kata ili kusogeza huduma bora ya afya Karibu na wananchi. Mhe Mabula amefafanua ofisi yake imepokea shillings 197,000,000 ambazo zimetumika kwenye miradi ya Maendeleo.

Mhe Mabula amewaambia wananchi wakati wa uchaguzi ilitolewa ahadi ya kutatua kero ya ardhi ambapo katika mitaa 11 ya Kata hiyo kupitia mpango Kabambe wamewezesha mitaa mitatu kupimiwa ardhi na wapo katika nazungumzo namna gani wananchi wanaishi katika maeneo  yenye changamoto ambapo watawekewa utaratibu wa upimaji shirikishi ili waweze kupimiwa ardhi.

Naye Diwani kata ya Isamilo Mhe Charlse Nyamasiriri amempongeza mbunge kupitia mfuko wa Jimbo ambavyo Umekuwa chachu katika sekta ya elimu Kata hiyo na amemshukuru Kwa namna anavyojitolea katika kushirikiana pamoja na wananchi wa Kata ya Isamilo amemwahidi ushirikiano zaidi katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi katani humo. 

Mkutano huo wa Mbunge na wananchi wa Kata ya Isamilo  umefanyika Mtaa  wa Nyakabungo C Kata ya Isamilo Mhe Mbunge Akiwa amembatana na mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana, watendaji serikali Kata na mitaa pamoja na mwenyeji  Diwani wa Kata hiyo Mhe Charlse Nyamasiriri.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana 🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: