Monday, 9 July 2018

Manji anarudi kwa kishindo Yanga


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ameweka wazi kuhusiana na mrejesho wa aliyekuwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji ambaye ombi lake la kuomba kujiuzulu lilipingwa na wanachama kuwa amekubali kurejea, imeelezwa.

Katika mkutano mkuu wa klabu uliofanyika Juni 10 kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam, idadi kubwa ya wanachama ilipinga barua hiyo na kuazimiwa wote kuwa inabidi aendelee kuwa Mwenyekiti.

Sanga ambaye amekaimu nafasi ya Manji, amefunguka na kusema kuwa wamejitahidi kufikisha kauli hiyo ya wanachama wa Yanga na akaeleza kuwa Mwenyekiti amekubali kurejea japo atahitaji muda kidogo.

Kwa mujibu wa Sanga aliyekuwa na viongozi wa matawi katika kikao, amesema hayo kuwa wameshafikisha taarifa hiyo kwa Manji na kuna uwezekano mkubwa akarudi kwa kishindi siku chache zijazo.

Wakati Yanga wakiendelea na jitihada za kumshawishi Manji arudi, timu ipo kambini hivi sasa ikijiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia Fc utakaopigwa Julai 18 jijini Nairobi.

No comments:

Post a Comment