Wednesday, 25 July 2018

Manara awataka Clouds FM waombe radhi baada ya kutangaza Simba wamefungwa goli 6-0 nchini Uturuki

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amekiomba kituo cha Radio cha Clouds FM kuomba radhi kwa mashabiki wa klabu hiyo kwa kutangaza kuwa wamefungwa goli 6-0 nchini Uturuki kwenye mchezo wa kirafiki.

Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa kama kituo hicho kitakataa kuomba radhi basi kithibitishe taarifa hizo kwani inaonekana ni ya uongo na inachafua brand ya Simba.

Ndugu zangu wa Clouds with do respect mnachotufanyia c haki na mnatukosea sana tena sana!! Leo mmetangaza kwenye Radio yenu Simba imecheza mechi Uturuki na kufungwa 6-0..tunaomba mthibitishe au mkanushe..vinginevyo mtakuwa na nia ovu ya kutudhalilisha na kwa hili hatutawaelewa na hatutakubali!! Mm wajibu wangu pia ni kulinda image ya Club yangu na sipo tayari kuona Chombo chochote kikitangaza taarifa ya uzushi na uongo dhidi ya Simba kwa kisingizio chochote kile..kwa hili nategemea mtachukua hatua stahiki haraka iwezekanavyo .vinginevyo thibitisheni @cloudstv @cloudsfmtz

Hata hivyo, mpaka sasa Clouds Media hawajaomba radhi wala kuthibitisha taarifa hizo kama ni za kweli au laah!.

Klabu ya Simba imeondoka wikiendi iliyopita kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2018/19 na ikiwa huko imeelezwa kuwa itacheza michezo kadhaa ya kirafik
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: