Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT-Wazalendo, wameingia makubaliano sita katika uchaguzi mdogo wa wa ubunge wa Jimbo la Buyungu na kata 77, unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

Makubaliano hayo yamefanyika baada ya mazungumzo na mashauriano ya viongozi wa pande zote mbili za vyama hivyo.

Katika makubaliano hayo vyama hivyo vimekubaliana kuwa ACT Wazalendo kitaiachia Chadema Jimbo la Buyungu na kushiriki kwenye kampeni na Chadema kitaiachia ACT Wazalendo Kata ya Gehandu (Hanang) na kushiriki kwenye kampeni.

Aidha, makubaliano mengine ni kwamba  Chadema kitaiunga mkono ACT Wazalendo kwenye kata ambazo ACT pekee kimegombea huku ACT Wazalendo kikiiunga mkono Chadema kwenye kata ambazo Chadema pekee kimegombea.

Makubaliano ya tano ni kwamba wagombea wa vyama vyote kwenye kata zilizosalia wataruhusiwa kuendelea na kampeni na sita ni ACT Wazalendo na Chadema vitashirikiana kukabiliana na hujuma kwenye kampeni, upigaji kura na utangazaji wa matokeo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: