Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amemfukuza kikaoni Kamishna Mkuu wa Magereza, Juma Malewa kwa kuchelewa.

Lugola amemfukuza Dk Malewa leo Julai 6, saa tano asubuhi ikiwa ni dakika chache baada ya kikao hicho kuanza.

Awali, Lugola alisema ikifika saa 5 kamili, mlango ufungwe na kama alivyoagiza, ulifungwa. Ilipofika saa 5:1 mlango ulifunguliwa ili Dk Malewa aingie.

Baada ya kuingia Dk Malewa, Lugola akahoji kwa nini amefunguliwa mlango?

Licha ya Dk Malewa kuomba msamaha, Lugola alikataa kata kata. Pia Lugola ameagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, kumshusha cheo hadi kubaki na nyota tatu, mkuu wa usalama barabarani, Mbeya, Leopold Fungu.

Pia ameagiza Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoa wa Kagera, George Mrutu ashushwe cheo.

Kikao hicho ni cha kimkakati cha viongozi wa vyombo na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: