Friday, 13 July 2018

KAIMU MTENDAJI KATA ASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UPOTEVU WA FEDHA, MIFUKO YA SARUJI 39

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara Elias Ntiruhungwa amemsimamisha kazi Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kenyamanyori  Laurent Marwa kwa upotevu wa fedha za Serikali pamoja na mifuko 39 ya saruji ambayo ilipaswa kujenga vyumba viwili katika Shule ya Sekondari Kenyamanyori.

Akizungumza leo, Mkurugenzi huyo amesema kuwa Kaimu huyo alienda kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkende na kusaini na kisha kukabidhiwa mifuko ya saruji huku akisubiliwa na wananchi waendelee na ujenzi katika Shule ya Sekondari Kenyamonyori.

Amefafanua lakini alitokemea kusikojulikna na mifuko hiyo.Pia  alipotea tena na sh.80,000 zilizochangwa katika mkutano wa hadhara na Diwani wa kata hiyo kwa ajili ya kuunga mkono wananchi katika ujenzi huo.Pia Mkurugenzi ameongeza kuwa viongozi wa Serikali ya kijiji walikaa na kupitisha mitasari ili Mtendaji huyo aweze kuchukua fedha benki Sh.590,000 lakini mpaka sasa hazijulikani fedha hizo zilipo baada ya kuzitoa benki.

Hivyo ameamua kumsimamisha kazi na kudai lazima afikishwe Polisi na baadae kufikishwa mahakamani ili  ajibu mashitaka yanayomkabili.“Nilimuita ofisini kwangu nikampa saa mbili ili arejeshe vitu hivyo mfano mifuko ya saruji na fedha hizo  lakini mpaka sasa hajarejesha chochote.Nimeamua kumsimamisha kazi na huyo akuna haja ya kuunda tume lazima kesho afikishwe Polisi na kufikishwa Mahakamani mara moja,"amesema Elias.

Mkurugenzi amesema kuwa nia ya Serikali ni kuweka mazingira bora ya wanafunzi ili wasome lakini baaadhi ya viongozi wasiokuwa na maadili wanazidi kufanya hujuma jambo ambalo hawatalifumbia macho.

Ameongeza watachukua hatua kali kwa wale wote ambao wanakiuka maadili.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na Vyombo vya habari ofisini kwake ambapo amesimamisha kazi Kaimu Afisa Mtendaji wa kata ya Kenyamanyori kwa sababu za ubadhilifu wa fedha za Serikali pamoja na Mifuko 39 ya saruji.

No comments:

Post a Comment