Wednesday, 25 July 2018

JWTZ LA ADHIMISHA KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA KWA KUFANYA USAFI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MONDULI

Mkuu wa shule ya Mizinga Sofa Kanali Julias Moses Gambosi na Mganga mkuu wa wilaya ya Monduli Dr.Titus Mmasi pamoja na askari wameshiriki kufanya usafi katika viunga vya hospitali na maeneo soko la kilasiku.

Akizungumza kanali gambosi katika siku ya mashujaa wao kama jeshi waliona vyema kuja kuadhimisha Siku hiyo kwa kushiriki kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli na amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kizalendo wa kufanya usafi katika mazingira yanao wazunguka.

Nae Mganga mkuu wa wilaya Dr. Titus Mmasi anashukuru jeshi la wananchi kwa kuja kufanya usafi katika hospitali yetu ya wilaya sio tu leo bali ni ushirikiano mzuri wa mara kwa mara jeshi kushiriki shughuli nyingi za kijamii na kuwatakia heri katika siku muhimu ya kumbukumbu ya Mashujaa.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: