Baada ya uongozi wa Yanga kumtambulisha kiungo Mohamed Issa ‘Banka’ kuwa imemsajili kwa mkataba wa miaka miwili, aliyekuwa ofisa habari wa klabu hiyo Jerry Muro amekosoa usajili huo.

Muro ali-comment kwenye ukurasa wa Instagram ya Yanga baada ya klabu hiyo kupost picha ya Banka akiwa amevaa jezi ya Yanga baada ya utambulisho comment ya Muro imelenga kukosoa usajili unaoendelea na kuonesha namna ambavyo haridhishwi na baadhi ya mambo yanavyokwenda.

“Hapa ndipo napojiuliza haya mambo yataisha lini awali tuliambiwa usajili ni kimyakimya, sasa naona mmeanza kutoa hadharani, haya tuendelee kuweka wengine hadharani.”

“Ila bado mnawasajili wachezaji dhaifu sana ambao hawaendani hadhi ya klabu kubwa kama Yanga. Hawa wachezaji wamechoka sana hawana tena uwezo, pumzi, akili na mbinu mpya hawa wanaelekea ukingoni mwa uchezaji wao.”

“Nawashauri Yanga hawa wachezaji mnasajili kwa ajili ya Yanga Veterans tu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: