Upande  wa Jamhuri umedai katika kesi inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake dhidi ya kesi ya mauaji ya dada wa bilionea huyo, Aneth Msuya kwamba jalada la kesi hiyo liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua za kikazi.

Kesi hiyo ilipangwa kutajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kwamba jalada liko kwa DPP likifanyiwa kazi.

Hakimu Simba aliilekeza Jamhuri itoe taarifa za jalada hilo tarehe ijayo. Mbali ya Miriam, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara Revocatus Muyela.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuwa Mei 25, 2016 walimuua kwa makusudi dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: