Monday, 23 July 2018

Jalada la Kesi ya Mke wa Bilionea Msuya lipo mikononi mwa DPP


UPANDE wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41) na mwenzake umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi hiyo bado lipo mikononi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kulifanyia uamuzi.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Patrick Mwita,  ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu,Thomas Simba,  kwamba anaomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine kwani jalada bado lipo mikononi Mwa DPP.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala,  amekubaliana na taarifa hiyo lakini akaomba jalada kufuatiliwa ambapo Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 30 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wanatuhumiwa kumuua kwa makusudi dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya,  tukio linalodaiwa kutokea Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a comment