Friday, 6 July 2018

Hatimaye Muna Akubali Kupeleka Msiba kwa Peter

Kufuatia  sintofahamu kuhusu nani ni baba halisi wa mtoto wa Muna na wapi msiba upelekwe, muigizaji Bongo Movies ambaye pia ni kiongozi wa tasnia hiyo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’  aliyeshiriki kupata ufumbuzi wa suala hilo, amesema hatimaye (Muna) mama wa mtoto marehemu Patrick, amekubali msiba upelekwe kwa baba wa marehemu ambaye ni  Peter Zacharia maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ‘Nyerere’ amesema amezungumza na Muna na kufikia maridhio hayo kwa pande zote za wazazi wa mtoto huyo.

Hayo yamejiri ikiwa ni baada ya kikao cha muda mrefu kati ndugu wa familia ya Muna na Peter kumsihi Muna ili waungane na baba wa mtoto huyo kufanikisha shughuli ya kumsitiri pamoja Patrick.

Mbali na Steve Nyerere, wasanii wengine waliokuwepo ni Shamsa Ford, huku Wema na mama yake wao walifika jana na kusema wasingeweza kwenda Mbezi kwa Muna kwani wanamfahamu Peter ndiye baba wa mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment