Thursday, 26 July 2018

Hamorapa Ajichora tatoo ya wema sepetu

Msanii wa hip hop Harmorapa ambaye anajizolea umaarufu kwa vituko vyake amefunguka na kudai anampenda Wema na amechora Tattoo mpya ya Jina lake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Harmorapa amefunguka na kudai mwanamke ambaye anajitangaza kuwa ataolewa na Harmorapa ni muongo kwa sababu hana Mahusiano naye.

Harmorapa amefunguka na kudai hana mpango wa kumuoa mwanamke aliyetoka Mwanza kwa ajili yake aliyejitambulisha kwa jina la Khadijah na kudai anataka kumuoa Wema.

Harmorapa amedai kwamba zile picha zinazosambaa Kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa ni clip za Kwenye Movie mpya ambayo amecheza naye lakini sio wapenzi.

Lakini pia Harmorapa amefungukia mapenzi yake kwa Wema Sepetu na kudai anampenda kupita kiasi na Yupo Tayari kumuoa muda wowote na hata kukiri kuchora Tattoo ya Jina na lake Kwenye shingo.

Siku za nyuma Wema ameshawahi kumtolea povu Harmorapa na kumtaka aache kujitangaza Kwenye vyombo vya habari kuwa anampenda kwani alikuwa anamkera.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: