Wednesday, 4 July 2018

Fedha za Ruzuku ni za Moto "Mwenyekiti Uvccm Arusha"  • Mwenyekiti waUmoja wa Vijana Ccm (Uvccm) Mkoa wa Arusha Ndugu Saitoti Zelothe sambamba na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Bi. Lulu Mwacha na Kamati ya Utekelezaji Mkoa Ameendelea na ziara yake mapema leo katika Wilaya Karatu  na kukagua shughuli mbalimbali za Kimaendeleo ikiwemo zoezi la uwezeshaji wa vijana katika wilaya hiyo.


Mwenyekiti  Ndugu Saitoti Zelothe ametoa onyo Kali kwa Viongozi wa UVCCM Wilaya zote za Arusha ,
"Hizi fedha za Ruzuku kutoka Mkoani tutakazo zileta ni fedha za moto zikiliwa lazima ucheue moshi huko tumboni hufuka kama nyama choma  hivyo basi MTU yoyote hatabaki salama atakayekula ama kuhujumu miradi ya Umoja wa Vijana Uvccm"

Pia Ndg. Saitoti Ameahidi kutoa Shilingi Milioni tano (5) kwa kila kikundi kitakacho rejesha marejesho katika mikopo iliyotolewa na halmashauri zao na kwenye miradi endelevu.

Hata hivyo Saitoti aliwakabidhi Vijana zaidi ya 80  Katika Wilaya ya Karatu kadi za Umoja wa Vijana na kuwaapisha kuwa wanachama wapya wa Ccm.

Pia ndugu Saitoti Zelothe amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli na kuwataka vijana kuenzi kazi hiyo kwa kuwa wazalendo na wachapakazi zaidi katika nyanja mbalimbali walizopo.

Ndg. Saitoti amewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kipindi hiki cha uchaguzi mgodo ili kuhakikisha wagombea wa ccm wanapita bila kupingwa ili  kuendelea kutekeleza ilani ya Ccm.


Mwenyekiti wa Uvccm mkoa wa Arusha amewataka vijana wa karatu kubuni miradi mbalimbali ili kuweza kupata mapato zaidi na kuacha kutegemea fedha kutoka katika ofisi ya umoja wa Vijana mkoa.


Sambamba na hapo Ndg. Saitoti amemtaka mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Karatu kuhakikisha wanaunda vikundi vngi vya Vijana ili kuweza kupata mkopo wa Asilimia 20% ya vijana inayotolewa na kila Halmashauri nchini.


 Ndg. Saitoti amewataka viongozi wote wa Wilaya kuhakikisaha kuwa ifikapo mwisho wa mwaka huu Makatibu wote wa CCm wilaya na Mkoa wana nyumba za kuishi, na kuhakikisha kuwa wanatafuta eneo na kuanza ujenzi mara moja 

Imetololewa na,

Omary Lumato
KATIBU HAMASA & CHIPUKIZI (M) ARUSHA

No comments:

Post a Comment