Tuesday, 3 July 2018

Familia ya Tundu Lissu kudai matibabu mahakamani

Wakati mbunge Tundu Lissu akiendelea na matibabu nchini Ubelgiji, kaka yake, Alute Mughwai amesema wanatarajia kwenda mahakamani kudai haki ya kisheria ya matibabu ya mbunge huyo.

Akizungumza jana Jumatatu Julai 2, 2018 na waandishi wa habari, Mughwai alisema wanachukua hatua hiyo baada ya Bunge kuiandikia barua familia hiyo, ikieeleza kuwa kuanzia sasa haitajishughulisha na matibabu ya mbunge huyo.

Mughwai alisema Juni 18, 2018  walipokea barua kutoka uongozi wa Bunge kuwa haitajishughulisha na matibabu ya mbunge huyo kwa kuwa yuko nje ya nchi kwa utaratibu binafsi.

“Limesema kwa kuwa anapatiwa  matibabu uko nje ya nchi kwa  utaratibu binafsi na hakufuata utaratibu wa matibabu,”alisema

Alisema kutokana na hali hiyo wanaangalia utaratibu wa kwenda mahakamani  kuangalia kama mwakilishi huyo anahaki kisheria ya  kupatiwa  matibabu.

No comments:

Post a Comment