Friday, 6 July 2018

Dogo Janja Apigwa Onyo


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abubakar Chande maarufu kama 'Dogo Janja' ameonywa na mwanamuziki mwenzake Belle 9, kwamba awe makini na Jiji la Dar es Salaam kwa madai lina watu wa kila aina ili asije kuharibiwa tabia yake ambayo yeye binafsi ameshindwa kuielewa kwa haraka.
Belle 9 ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana baada ya Dogo Janja kudai Belle anapaswa kupigwa viboko 70 kwa kile alichokidai kudharau wakubwa zake akiwa anamlenga Baba yake mlezi Madee Ali.
"Tuna tofautiana katika kufikiri baina yangu na Dogo Janja unajua zama za viboko zimeshapitwa na wakati, halafu unajua kabla hajaachia huu wimbo wake mpya nilikuwa nasikiliza ule wa zamani ambao alijifanya kama dada hivi lakini pia sasa hivi ameachia ngoma mpya anasema 'your my banana",amesema Belle 9.
Pamoja na hayo, Belle ameendelea kwa kusema "hakuna mtu asiyejua maana ya 'banana' hii imekaa kiutata kabisa, sasa hapo viboko labda yenye mwenyewe ndio anapaswa apigwe kwasababu nashindwa kumuelewa. Madee amchunge mtoto wake mjini hapa maana kuna watu wa aina tofauti". 

No comments:

Post a Comment