Thursday, 5 July 2018

Diwani Mwingine wa Chadema Geita Ajiunga na Ccm

Diwani pekee wa Chadema kata ya Bugalama, Luponya Masalu amejivua uanachama na kutangaza kujiunga na CCM.

Alikuwa ni diwani pekee wa Chadema katika baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Masalu amesema ameamua kurudi CCM baada ya kuona Rais John Magufuli anatekeleza mambo aliyokuwa akiyasemea akiwa Chadema.

“Sijanunuliwa wala kutishwa kama baadhi ya wananchi wanavyodai na  hakuna mwenye uwezo wa  kunihonga lakini nimehama kutokana na utendaji kazi nzuri ya Rais Magufuli,” amesema

Kuhusu kugombea nafasi hiyo wakati mwingine Luponya amesema kwa sasa hawezi kuzungumzia hilo na kwamba atakapotulia atafanya maamuzi kama atagombea tena.

No comments:

Post a Comment