Monday, 2 July 2018

Diwani Munisi Awataka Vijana kufanya kazi kwa bidii


Na mwandishi wetu Ester Bhoke

Diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Martin Munisi, amewataka vijana kusoma na kufanya kazi kwa bidii  huku wakimtanguliza Mungu mbele.

Munisi ameyasema hayo jana wakati akizungumza na  vijana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Woongo, Kata ya Machame Magharibi ambao wameungana na vijana wenzao wa kanisa hilo kuhitimisha mwezi wa vijana.

Katika maadhimiho hayo, kwa muda wa mwezi mzima vijana hao 250 wamejishughulisha na kazi za mikono zikiwamo kuotesha miti ya miparachichi ya kisasa, miti ya mazingira na maua na kujenga ukuta wa kanisa hilo.

Aidha, Diwani huyo ambaye pamoja mambo mengine pia alizindua Mfuko wa Vijana kwa ajili ya mradi wa duka na huduma ya M-Pesa.

Katika harambee hiyo, jumla ya Sh milioni 3.5 zilipatikana.

Pamoja na mambo mengine, Munisi amewashukuru marafiki waliomsindikiza na kufanikisha harambee hiyo ambao ni Mjumbe wa NEC, Anthony Maswi na Mkurugenzi Kmpuni ya Simu za Mkononi ya Halotel, Kanda ya Kaskazini, Omar Lumato.

No comments:

Post a comment