Saturday, 14 July 2018

DC HOMERA ARIDHISHWA NA MWENENDO WA UJENZI WA GHALA LA KUHIFADHIA KOROSHO LINALOJENGWA NA SERIKALI YA CCM KUPITIA BODI YA KOROSHO TANZANIA (CBT).Kwa Tsh.Billion 5.7


Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma aliyasema hayo alipokuwa amekwenda kutembelea mradi huo unaojengwa na kampuni ya wazawa Skycity ya Dar es salaam Tanzania.

Aidha DC Homera aliwapongeza na kuwataka wamalize ujenzi wa mradi  huo kwa wakati kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa kati ya CBT na mkandarasi huyo ,Ghala hilo lina urefu wa mita 135  na upana mita 35  linatarajia kuhifadhi korosho Tan 15000 mpaka 20,000 kwa wakati mmoja.

Hata hivyo DC Homera alisema ghala hilo mpaka kukamilka kwake  litagharimu fedha za Kitanzania Tsh Billion 5.7 , aidha Homera alieleza kwamba ghala hilo litapunguza kwa kiwango kikubwa wizi wa rejareja wa korosho za wakulima Mara wafikishapo ghalani kuu kwaajili ya mnada wa korosho hizo,pili kutawawezesha wakulima kuwahi soko lenye bei nzuri  kwakuwa korosho zao zitawahi kuondolewa shambani na kufikishwa ghala kuu.

DC Homera aliwaomba Bodi ya korosho CBT kupitia kaimu mkurugenzi mkuu wake wa (CBT) Prof. Wakuru Magigi  kuwa nae bega kwa bega mkandarasi huyo ili amalize kazi yake kwa  wakati.

No comments:

Post a Comment