Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amelipongeza shirika la Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhamasisha masuala ya elimu katika mkoa wa Arusha na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo. Alitoa pongezi hizo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini Arusha, ambapo Taasisi hiyo iliandaa Tuzo maalumu kwa mwalimu bora .(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo ,iliyofanyika hivi karibuni katika shule ya Levolosi jijini Arusha,ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa wameaanda Tuzo hiyo kwa shule za msingi jiji la Arusha na Meru kwa walimu 20
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya sombetini,Caroline Kiyoja cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingi laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Sinoni,Dorice Mhina cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingili laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation For Tomorrow 
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Levolosi,Elizabeth Minja cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingi laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Uhuru,Jane Mkomwa cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingi laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Lucky Vicent Julius Saunyi cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingi laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation For Tomorrow
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akimkabidhi Mwalimu wa shule ya msingi Daraja mbili Leah Mshana cheti cha mwalimu bora sanjari na shilingi laki moja na nusu kama motisha kwa walimu ambao wanafanya kazi zao kwa umahiri mkubwa, Tuzo hiyo maalumu imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation For Tomorrow
Walimu kutoka shule za msingi jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya cheti pamoja na kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja Tuzo hiyo maalumu iliandaliwa na shirika la Foundation For Tomorrow kwaajili ya waalimu waliobainika kufanya kazi zao kwa umahiri mkubwa

*****

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la Foundation For Tomorrow kwa kazi nzuri linayoifanya katika kuhamasisha masuala ya elimu katika mkoa wa Arusha.

Aliyasema hayo juzi katika Juma la Elimu katika shule ya msingi Levolosi jijini Arusha ambapo alisema shirika hilo limekuwa bega kwa bega katika kuhamasisha maswala mbalimbali ya Elimu na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuiga mfano huo

“Foundation for Tomorrow wamekuwa mstari wa mbele sana katika maswala ya elimu mfano mzuri leo wameandaa Tuzo maalumu kwa mwalimu bora ambaye amekuwa akifanya kazi zake kwa umahiri mkubwa”,alisema Daqarro.

Kwa upande wake Meneja wa programu ya mafunzo kwa walimu Noah Kayanda kutoka shirika la Foundation for Tomorrow akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa lengo la Tuzo hiyo ni kutia hamasa miongoni mwa walimu waliobainika kufanya kazi zao kwa bidii na umahiri mkubwa.

Alisema katika zoezi hilo la kumsaka mwalimu bora limezingatia vigezo vyote ikiwemo uwezo wa kuhamasisha ufikiri wa kina miongoni mwa wanafunzi,uwezo wa kutengeneza mazingira ya kushiriki na mazingira rafiki ya kujifunza,uvumbuzi na ubunifu katika swala zima la ufundishaji na utekelezaji wa mtaala.

Kayanda aliongeza kuwa vigezo vingine ni pamoja na kujikita katika kusaidia watoto wenye changamoto za kujifunza pamoja na uzoefu wa kujifunza.

Alisema kuwa katika Tuzo hiyo ya mwalimu bora kila mwalimu atapewa zawadi ya cheti pamoja na kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja. 
Na Pamela Mollel,Arusha
Share To:

msumbanews

Post A Comment: