Sunday, 8 July 2018

CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya ambaye ytuko upande wa Profesa Lipumba  amesema chama hicho kitashiriki uchaguzi wa ubunge katika majimbo ya Buyungu, Jangombe na kwenye Kata 79.

Akizungumza jana Sakaya alisema chama hicho kimepokea barua kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kikielezwa kuwa majimbo na kata hizo, yapo wazi.

Alisema kutokana na mabadiliko yaliyofanyika NEC na katika vyombo vya Dola ni wazi kuwa wataibuka na ushindi katika chaguzi hizo

“Naomba ifahamike kuwa CUF ipo moja na uamuzi wa chama ni kushiriki uchaguzi,  wanachama wasisikilize maneno ya watu ambao hawahusiki na chama," alisema Sakaya.

Alisema wapo wanaojitambulisha kuwa viongozi wa CUF wanasema hawatoshiriki, si kweli wamachama  na wenye nia ya kutaka kugombea ubunge na udiwani wajitokeze.

"Uchaguzi wa ubunge jimbo la Kinondoni tulilalamikia utaratibu ulivyokuwa na namna NEC walivyokiuka. Ila kw amabadiliko yaliyofanyika sasa, naamini hali itakuwa nzuri,” alisema Sakaya.
 
Pia nae Profesa Ibrahim Lipumba amewataka wanachama kuzipuuza habari kuwa wamesusia kushiriki chaguzi hizo

No comments:

Post a Comment