Monday, 30 July 2018

Alikiba kukosa mechi muhimu Coastal

MSHAMBULIAJI mpya wa Coastal Union ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, AliKiba huenda akakosa mechi za awali za Ligi Kuu Bara kutokana kubanwa na majukumu ya kupiga shoo.

Ligi Kuu imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22 lakini ratiba ya shoo ya Alikiba inaonyesha itaanza Agosti 17, 18 na 25, mwaka huu huko Toronto, nchini Canada katika shoo iliyopewa jina la The All Star Music.

Ratiba inaonyesha Coastal Union wataanza ligi, Agosti 22 dhidi ya Lipuli FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga hivyo Alikiba hatokuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mechi hiyo.

Meneja wa Coastal Union, Said Hilal alisema kuwa, wanatambua majukumu ya Alikiba hivyo haina shida kwani wana wachezaji wengine ambao wataziba nafasi yake.

“Tunajua AliKiba ana majukumu yake mengi na sisi kama klabu hatuwezi kumzuia kwenye hilo pale ambapo atakuwepo atafanya kazi na wenzake hivyo hakuna tatizo,”alisema

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: