Monday, 30 July 2018

AGIZO LA RAIS MAGUFULI KUHUSU FEDHA ZA MASHUJAA KUTUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA LATEKELEZWA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akiogea na Mkandarasi wa kampuni ya Mionzi Jua, Christopher Athumani, wakati alipofika kukagua kazi inay fanywa na  kampuni hiyo ya kuweka taa kwenye barabara ya Emmaus-African Dream jijini Dodoma, wengine ni Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe (mwenye koti).


Muonekano wa baadhi ya Taa za barabarani zinazowekwa katika barabara mpya ya Emmaus-African Dream jijini Dodoma, Taa hizo zinawekwa kufuatia agizo la Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli, aliyetaka fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa mwaka huu, kiasi cha Shilingi milioni 308, zitumike kuboresha miundombinu ya barabara za jiji hilo.

Muonekano wa taa ya kuongoza magari katika makutano ya barabara mpya ya Emmaus-African -Dream jijini Dodoma. Taa hiyo imewekwa kufuatia agizo la Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli, aliyetaka fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa mwaka huu, kiasi cha Shilingi milioni 308, zitumike kuboresha miundombinu ya barabara ya jiji hilo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: