Saturday, 7 July 2018

ACT-Wazalendo kushiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Buyungu na Kata 79 ........ Watangaza ushirikiano na wapinzani

Chama cha ACT- Wazalendo kimetangaza kushiriki kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Buyungu na Kata 79 huku kikibainisha kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani.

Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara), Shaaban Mambo amesema uamuzi huo umefikiwa na kikao cha Kamati Kuu baada ya kufanya tathmini.

Akizungumza leo Julai 7, 2018 Mambo amesema kamati imeona umuhimu wa chama hicho kushiriki katika uchaguzi huo kwa lengo la kujijenga zaidi.

Amesema ACT wapo tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani kwa kusimamisha mgombea mmoja ili kushindana na CCM.

"Tunaamini kuwa watu watatumia uchaguzi huu kuonyesha hasira yao dhidi ya serikali ya CCM, ndiyo sababu tupo tayari kushirikiana na vyama vya upinzani,"

"Ushirikiano wetu ni kwenye kuachiana wagombea katika maeneo ambayo tunaona chama fulani kinafanya vizuri,” amesema

Amesema katika kata 79, ACT ina uhakika wa kufanya vizuri katika kata 30 lakini itakuwa tayari kuachia chama chochote cha upinzani endapo itathibitika kuwa mgombea wake ni mzuri kuliko wao.

No comments:

Post a Comment