Saturday, 9 June 2018

Zari: “Hamisa Hata Akitaka Kuzaa Watoto Kumi na Diamond Azae Tu”

Mfanyabiashara maarufu na mama watoto wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan amemwaga povu na kusema Hamisa hata akitaka kumzalia watoto kumi Diamond yeye kwake ruksa.

Zari ametoa kauli hiyo jana baada ya kuweka posti yake aliyokuwa anasherehekea kufikisha followers milioni 4 Kwenye mtandao wa Instagram ambapo shabiki alimtahadharisha kuwa kuna tetesi Hamisa ana ujauzito mwingine.

"Zari kuwa makini kuna tetesi huku mtaani kwetu kuwa Hamisa kashanasa mimba nyingine ila lisemwalo lipo kama halipo laja”.Aliandika shabiki huyo

Baada ya kupewa maneno hayo Zari alimjibu hata wangezaa watoto kumi yeye hana habari kwani hayumo.

Zari alijibu kwa kuandika:" Azae hata kumi mimi simo!”.

Huu ni muendelezo tu wa drama iliyoanza mwaka jana baada ya Hamisa kubeba mimba ya  Diamond

Kumekuwa na tetesi  kuwa Diamond amerudisha majeshi kwa mama watoto wake Zari baada ya kuachana na  kutoonana kwa muda mrefu

No comments:

Post a Comment