Wednesday, 6 June 2018

Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako alivyomwaga machozi msiba Maria na Consolata

Miili ya mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (20) waliofariki dunia Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, imeagwa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) kabla ya kuzikwa katika makaburi ya viongozi wa dini yaliyopo Tosamaganga mkoani humo leo Jumatano, Juni 6, 2018.

Maria na Consolata ambao enzi za uhai wao walikataa kutenganishwa, watazikwa kwenye jeneza moja litakalokuwa na misalaba miwili.

Familia za baba na mama wa mapacha hao kutoka Tukuyu, Mbeya na Bukoba, Kagera, waliokuwa walezi wa mapacha hao, masista wa Consolata wa Iringa, na waombolezaji wengine,  wameungana katika kuwasindikiza mapacha hao katika safari yao ya mwisho duniani.

Pia viongozi mbalimbali wa kimkoa na wa kitaifa wameungana na waombolezaji  kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa pacha hao, Maria na Consolata Mwakikuti.

Miongoni mwa waliofika ni pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Willium. 

No comments:

Post a Comment