Saturday, 9 June 2018

Waziri Nchemba - Kwa Simba hii naipa baraka


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Mwigulu amesema kwa sasa anachoweza kukielezea kwa timu ya Simba anamuomba Mungu aifanikishe timu hiyo kushinda mchezo wa fainali wa michuano ya Sport pesa dhidi ya timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya.

Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wametinga fainali ya michuano hiyo na kesho Jumapili watacheza mchezo wa fainali ya michuano hiyo na timu ya Gor Mahia ya Kenya.

Akizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Saalam jana Dk.Mwigulu amesema amefurahi Simba kuingia fainali na sasa anatoa baraka ili ishinde kombe la michuano hiyo.

Michuzi Blog baada ya kukutana na Waziri Mwigulu pamoja na mambo mengine ilitaka kufahamu nini kauli yake kwa Simba inayosubiri kucheza fainali hiyo."Kwangu niseme tu naipa baraka zote timu ya Simba ili ishinde kombe la michuano hiyo.Hiki ndicho nachoweza kukielezea kwa sasa.

"Mashabiki wa soka nchini Kenya baada ya mwaka jana moja ya timu yao kuchukua kikombe hicho walitoa maneno ya kutubeza sana lakini tunaka kuonesha tupo vizuri.Hata hivyo nilitamani sana Simba icheze fainali na Singida United lakini imeshndikana,"amesema.

Alipoulizwa kwanini alitamani Simba icheze fainali hiyo na Singida United akafafanua maana yake ni moja tu kombe la michuano hiyo lingebaki Tanzania kwa asilimia 100.

"Fainali ingekuwa kati ya Singida United na Simba tungekuwa na uhakika tayari kombe la michuano hiyo ni la kwetu maana timu yoyote ambayo ingelichukua ilikuwa inaleta kombe nyumba,"amesema Dk.Mwigulu.

Mashabiki wa soka nchini Tanzania na hasa mashabiki wa Simba wameonesha matumaini makubwa na timu yao kuwa itaibuka mshindi na kuchukua kombe hilo.

No comments:

Post a Comment