Wednesday, 6 June 2018

Waziri Mwigulu Aagiza Jeshi la Polisi kupitia Upya Mikataba


Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dkt.Mwigulu Nchemba aagiza jeshi la polisi kupitia upya mikataba ,bei na ubora wa vifaa wanavyoagiza nje ya nchi kwaajili ya matumizi ya jeshi hilo ili kuleta usawa wa dhamani ya fedha na bidhaa wanazoagiza.

Ameyasema hayo leo mara baada yakufanya ziara ya kustukiza katika bohari ya Polisi Kurasini na bandari ya Dar es salaam ambapo amebaini kuna  baadhi ya vitu vya jeshi hilo vikiwemo vitambaa vya sale za nguo za polisi na magari  vimezuiliwa baada yakuonekana vina mkanganyiko katika uagizwaji wake na kushindwa kitoleea kwaajili ya matumizi.

Amesema kwa vitu ambavyo viliagizwa na kuonekana vimechelewa kufika kutokana na uzembe wa mzabuni zichukuliwe hatua kisheria ili kukomesha tabia hiyo ambayo imekua ikijirudia na kusababisha hasara nchini.

Ametoa muda usiozidi wiki tatu kwa jeshi hilo kumpatia ripori ya vifaa vyote vya jeshi vilivyoagizwa na vikashindwa kupita kwa wakati ili wabaini mapungufu yako wapi hali itakayowafanya kuchukua hatua za haraka ili kuokoa fedha za serikali ambazo zinatokana na wanachi kulipa kodi kwenye huduma mbalimbali za kijamii.

No comments:

Post a Comment