Tuesday, 5 June 2018

Wakati wa Manji mishahara ililipwa kwa wakati na timu ilifanya vizuri – Clement Sanga

Naimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amedai wakati aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji yupo madarakani klabu hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa sana.
Sanga miongoni mwa mambo ambayo aliyadadavua kwa upana ni maisha ya Yanga kabla na baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji.
“Tunashukuru kwa alichofanya Manji katika kipindi chote ambacho alikuwa madarakani na kabla ya kuwa madarakani wakati huo akiwa mdhamini wa klabu, amekuwa ni msaada mkubwa. Kila mwanachama na mpenzi wa Yanga anajua maisha tuliyokuwa nayo wakati huo, Manji alikuwa mpiganaji na timu iliweza kufanya vizuri kwa kipindi chote ambacho alikuwepo.,” Sanga alikiambia kipindi cha SportXtra cha Clouds FM.
Aliongeza,”Katika kipindi cha hivi karibuni wakati Manji yupo Yanga tuliweza kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kambi mbalimbali hakukuwa na tatizo la kulipa mishara, ilikuwa inalipwa kwa wakati. Aina ya wachezaji na benchi la ufundi lilikuwa ni zuri sana katika vipindi vyote ambavyo alikuwepo na hakukuwa na dosari.”
Klabu hiyo yenye makazi yake Jangwani jijini Dar es salaam imekuwa na matokeo mabaya toka Manji aondoke madarakani. Wiki hii katika michuano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya klabu hiyo imeondoshwa kwa kipigo cha goli 3-1 dhidi ya timu inayoshika mkia katika ligi ya Kenya.

No comments:

Post a Comment