Wahanga watatu wa tiba iliyodaiwa kutibu Virusi vya  UKIMWI ya aliyekuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh wamemshitaki Rais huyo aliye uhamishoni kwa kudai kuwa haki zao za kibinadamu zilivunjwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa African News, umesema kuwa Wahanga hao waliojulikana kama Ousman Sowe, Lamin Ceesay, na Fatou Jatta madawa hayo yalisababisha hali zao kuwa mbaya na wengine kupoteza maisha.
Aidha wahanga hao wameweka bayana kwamba awali walikuwa na uoga wa kumshitaki akiwa Rais lakini sasa ukweli lazima ujulikane.

Wahanga hao wamedai kuwa tiba hiyo iliwaathiri sana kisaikolojia kwani wakati mwingine aliwapaka dawa za mafuta katika vipindi vilivyooneshwa kwenye televisheni.

Rais Yahya Jammeh alianzisha tiba hiyo ya asili mwaka 2007 akidai inatibu UKIMWI. Tiba ambayo iliwataka wagonjwa hao kuacha kunywa dawa za kupunguza makali ya VVU za ARV na kunywa madawa ya asili yaliyowasababishia kutapika.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Programu hiyo mbadala ilirudisha nyuma harakati za kupambana na ugonjwa wa UKIMWI katika nchi hiyo ambayo iko nyuma katika viwango vya tiba kwa mujibu wa UNAIDS.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: