Saturday, 9 June 2018

Vyuo 20 vyafutiwa usajili na NACTE

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE),limetengaza kufuta usajili wa vyuo 20 baada ya kubaini vimeshindwa kufuata tararibu zinazoendana na matakwa ya usajili wa vyuo nchini.
Kaimu Katibu NACTE, Dkt. Adolf Rutayunga akizungumza na wanahabari alisema uamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia kifungu cha 20 cha kanuni za usajili wa vyuo vya ufundi 2001.
“Baraza limefuta usajili wa vyuo 20 baada ya kugundua kuwa vimeshindwa kufuata utaratibu zinazoendana na matakwa yanayoendana na usajili wa vyuo hivyo, na uamuzi huu umefanyika kisheria kwa kuzingatia kifungu namba ishirini kwa kanuni ya usajili wa vyuo vua ufundi zilizotungwa mwaka 2001,” amesema Rutayunga.
vyuo vilivyofutiwa usajili ni pamoja Covenant College of Business Sdudies(Dar es Salaam), Mugerezi Spatial Technology College(Dar es Salaam),Techno Brain(Dar es Salaam), DACICO Institute of Business and Management(Sumbawanga) na Arusha Institute of Technology (Arusha).
Aliendelea kuvitaja vyuo vingine ni Lisbon Business Collage(Dar es Salaam), PCTL Training Institute(Dar es Salaam), Royal College of Tanzania(Dar es Salam), Iringa RETCO Business College(Iringa) na Highlands Health Instutute(Njombe), East African Institute of Entrepreneurship and Finacial Management(EAIEFM) (Arusha), Musoma Utali Collage (Shinyanga) na Mlimani School of Professional Studies(Dar es Salaam).
Pia kuna chuo cha Dinobb Institute of Science and Business Technology(Mbeya), Institute of Social Work(Mbeya), Regency School of Hygiene (Dar es Salaam), St.Peters College of Health Sciences(Dar es Salaam), Genesis Institute of Social Science(Dar es Salaam), Institute of Management and Information Technology(Dar es Salaam) na Boston City Campus of Business College(Dar es Salaam).

No comments:

Post a Comment