Monday, 4 June 2018

Uwoya afunguka Ishu ya kuifuta Tatuu ya Masogange


MKALI wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya ameeleza juu ya madai ya watu wanaosema kuwa ameifuta tatuu ya aliyekuwa video queen maarufu Bongo, marehemu Agness Gerald ‘Masogange’ na kusema kuwa ni kitu gani kinachoweza kumfanya aifute tatuu hiyo?

Uwoya aliiambia Over Ze Weekend kuwa, aliichora tatuu hiyo kwa kuwa ni jambo lililotoka moyoni mwake na lilitokana na uchungu aliokuwa nao wa kupitiliza kwa rafiki yake huyo hivyo hawezi kuifuta.

“Nitaanzaje kuifuta? Ni kitu ambacho nime-kichora mwen-yewe, tena cha kumbukumbu muhi-mu kwenye maisha yangu, jamani itaendelea kudumu kwenye mkono wangu daima,” alisema Uwoya ikiwa ni zaidi ya siku 40 tangu Masogange afariki dunia.

No comments:

Post a Comment