Wito umetolewa  wanakijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga kuacha kushiriki kwenye biashara za magendo badala yake watumie maeneo yaliyorasmi kisheria kwa ajili ya upitishaji wa bidhaa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo wakati akizungumza na wananchi  kwenye mkutano uliofanyika eneo la sokoni akiwa ameambatana na maafisa wa TRA Mkoani Tanga.

Alisema kitendo cha wananchi kuacha kutumia bandari ya Pangani ambayo ipo kisheria wanafanya makosa makubwa na kuwataka kuitumia kupitisha bidhaa badala ya kutumia zile ambazo hazitambuliki ambazo watakapokamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria.

“Tumefika hapa kigombe kutoa elimu kwa kuzungumza na wananchi kutokana na changamoto za mara kwa mara biashara za magendo ambazo zimekuwa zikipitishwa eneo hilo na kuona kutumia muda huo kuzungumza na wananchi kuwaambia madhara yake ni yapi”Alisema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: