Monday, 4 June 2018

TFF yafuata utaratibu wa FIFA


Shirikisho la soka nchini (TFF), limefuata utaratibu ambao Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA), hutumia ili kusikiliza vyama wanachama wa shirikisho hilo kupata maoni kwaajili ya kuboresha utendaji kazi kwa maendeleo ya soka.

Kamati ya Utendaji ya TFF, ambayo ilikuwa jijini Arusha kwaajili ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC), imefanya kongamano kubwa la (TFF Executive Football Summit 2018) lililowakutanisha viongozi wa soka kutoka mikoa 6 nchini.

Kongamano hilo lililoongozwa na Rais wa TFF Wallace Karia jana Juni 3, Mkoani Arusha, limejadili mambo mbalimbali ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya michezo pamoja na vyama vya mikoa kuwekeza nguvu kwenye soka la vijana.

Wajumbe waliohudhuria 'TFF Executive Football Summit 2018', ni kutoka mikoa ya Singida, Dodoma, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na wenyeji ambao ni Mkoa wa Arusha.

Mapema Mwaka huu FIFA ilifanya Kongamano kubwa kwa nchini wanachama zaidi ya 17 barani Africa na lilifanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Rais wa FIFA Gianni Infantino pamoja na Rais wa CAF Ahmed Ahmed.

No comments:

Post a Comment