Saturday, 9 June 2018

TeamKiba Yakubali Kichapo cha 4-2 dhidi ya Teamsamatta


Kikosi cha TeamKiba kimekubali kichapo cha mabao 4-2 dhidi ya TeamSamatta katika mchezo maalum wa kuchangia fedha kwa ajili ya vifaa vya kujifunzia wanafunzi uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ilianza kwa kasi ambapo TeamKiba walianza na kasi kubwa mshambuliaji Ibrahim Ajibu alitikisha nyavu mara mbili ndani ya kipindi cha kwanza.

Mohammed Samatta aliipatia TeamSamatta alisawazishia  bao la kwanza na kuweza kufanya dakika 45 za kwanza kumalizika kwa TeamKiba ikiwa mbele kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa TeamSamatta kuja juu zaidi ikilishambulia lango la TeamKiba na kuweza kujipatia mabao matatu kupitia kwa Haruna Moshi 'Boban', Jamhuri Julio na Mbwana Samatta.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, TeamSamatta ilikuwa 4, TeamKiba 2.

No comments:

Post a Comment