Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Joseph Mbilinyi (Sugu) ameitaka Serikali kuwasaidia askari magereza wanaostaafu kulipwa mafao bila ya usumbufu kwani wanapostaafu husubiri hadi zaidi ya miaka miwili.

Ameyasema hayo leo Juni 4 bungeni, Sugu amesema Serikali huwasumbua askari hao bila sababu za msingi wakati wanafanya kazi ngumu ya kuwatunza wahalifu.

“Mheshimiwa spika, serikali inasema kuhusu askari hawa ambao wamekuwa wakisumbuliwa kutolipwa stahiki zao baada ya kustaafu wakati polisi wanaotukamata na kutupiga wanalipwa mapema lakini wahalifu wote wanarundikwa magereza kwa hiyo hawa wanakuwa na kazi ngumu,” amesema Sugu.

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kuwa swali hilo licha ya kuwa ni refu lakini ameamua kuliacha lijibiwe kwani limeulizwa na mtu mzoefu kuliko maswali mengine yanayoulizwa kwa ubabaishaji.

Akijibu swali hilo na swali la msingi kutoka kwa mbuge wa Viti Maalum Lucy Mlowe (Chadema), Naibu Waziri wa Fedha Dk Ashatu Kijaji amesema Serikali inalipa mafao kwa wastaafu wote bila ya upendeleo na kuwa katika kipindi cha hivi karibuni, zililipwa jumla ya Sh 282 bilioni kwa wastaafu mbalimbali.

Naibu waziri amewaondoa hofu pia watumishi wote walioajiriwa katika miaka ya 1980 kupitia Serikali Kuu lakini wakati ule hapakuwa na makato ya mfuko wa kijamii.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: