Saturday, 9 June 2018

SPORTPESA KUTOA MILIONI 250 KAMA BONAZI KWA BINGWA KAGAME, NI KWA TIMU INAZOZIDHAMINI TUWakati Yanga ikituma barua ya maombi kuelekea TFF ikiomba kujiondoa kwenye mashindano ya KAGAME yanayotaraji kuanza Juni 28 2018, Imeelezwa kuwa SportPesa wameahidi bonazi kwa mshindi wa taji hilo.

Taarifa zimeeleza kuwa mabosi wa kampuni hiyo ya bahati nasibu imeahidi kitita cha bonazi ya shilingi milioni 250 kwa timu ambayo iliyo chini ya udhamini wake endapo itabeba kikombe.

Michuano inayoanza Juni 28 itashirikisha jumla ya timu nne ambazo zipo chini ya udhamini wa SportPesa, timu hizo ni Yanga SC, Simba SC, Gor Mahia FC na AFC Leopards.

Yanga ni miongoni mwa timu hizo lakini endapo kama itashiriki kutokana na kutuma maombi kwenda TFF ikiomba kujiondoa kwa sababu ilizozieleza kuwa inahitaji kuwapa mapumziko wachezaji wake.

Endapo Simba watafanikiwa kutwaa ubingwa wa Kagame watakuwa wamelamba bonazi ya pili baada ya ile milioni 100 waliyochukua kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment